Magoli kutoka kwa Will Keane na Pereira yaliipa Man
United mwanzo mzuri katika maandalizi ya msimu wanapo jipanga kuikabili
Borussia Dortmund huko Shanghai
Jose Mourinho amesisitiza kuwa kinda la Manchester United Andreas
Pereira ana kipaji kukubwa baada ya kuonesha uwezo United ikishinda 2-0
dhidi ya Wigan Athletic.Mbrazili huyo aliingia kipindi cha pili baada ya Mourinho kufanya mabadiliko saba katika uwanja wa DW na alifanya kazi nzuri kumshawishi bosi wake mpya.
Magoli kutoka kwa Will Keane na Pereira yaliipa Man United mwanzo mzuri katika maandalizi ya msimu wanapo jipanga kuikabili Borussia Dortmund huko Shanghai.
Akizungumzia ufanisi wa mchezaji huyo, Mourinho alidai kuwa Pereira ana uwezo mkubwa, maono na mbinu.
"Andreas ana vipaji vingi," alisema. "Ana mbinu na maono ya kipekee," aliongeza Mourinho.
"Hivyo naongelea wachezaji wawili ambao kwa uhalisia ni watoto, bila ya presha na katika mazingira tulivu na hawajatisha zaidi lakini wapo vizuri."
Louis van Gaal alisitisha uhamisho wake wa mkopo msimu uliopita lakini hakuweza kupata muda wa kucheza na hali hiyo ilimfanya kinda huyo kuwa na jazba nyingi Old Trafford.
Mourinho anaelewa uwezo wake na goli lake limedhihirisha uwezo wake kufanya maajabu dimbani kwa kuupeleka mpira kwenye kona ya juu kwa shuti lake la kwanza.
Tumaini lipo kwamba atapata fursa katika kikosi cha Mourinho msimu huu, lakini uhamisho wa mkopo ungemsaidia pia kwa sababu anastahili kupewa muda wa kutosha dimbani.
0 comments:
Post a Comment