Jose Mourinho amesisitiza kwamba hawezi kujaji wachezaji wake wa
Manchester United kutokana na kipigo cha mabao 4-1 walichokipata kutoka
kwa Borussia Dortmund na kusema kwamba: “Injini ilikuwepo ilikuwa ni
tofauti kabisa, iliku ni kati ya Formula One against Formula Three”
“Mawazo yangu ni rahisi mno,” alisema Mourinho. “Najua kwamba wakati huu
wa pre-season timu ambayo iko vizuri kwenye maandalizi lazima iwe
vizuri zaidi ya rimu nyingine.”
“Hii hutokea kila mwaka. Baadhi ya timu bora hupoteza kwa magoli mengi.
Nadhani hili lipo wazi kabisa. Baada ya dakika 10, tulianza kujua kwamba
timu moja ilianza mazoezi siku 10 zilizopita na kucheza mchezo mmoja na
nyingine ilianza mwezi mmoja uliopita na imeshacheza michezo minne. Ni
rahisi mno kuona kuona utofauti wa ugumu wa mchezo na umakini wa
wachezi. Kwa upande wetu ulikuwa ni mchezo mgumu sana.
Kipindi cha pili tulikuwa wazuri na kuuzoea zaidi mchezo. Nadhani
matokeo ya mabao 3-2 yangekuwa sahihi zaidi ya 4-1 lakini Dortmund
walionesha ubora mkubwa waliokuwa nao, kwa mchezaji mmoja-mmoja na timu
nzima. Walionesha kwamba walikuwa wameshapiga hatua kubwa kwenye mazoezi
zaidi yetu.
Alipoulizwa kama angewajaji wachezaji wake kutokana na mchezo ule,
Mourinho akajibu: “Mimi nadhani ni muunganiko wa sababu vitu mbalimbali.
Lakini kwa kuzungumzia uhalisia wenyewe, sidhani kama naweza kuwafanyia
tathmini ilhali kulikuwa na utofauti mkubwa kati ya timu hizi. Kwa sasa
injini zina utofauti mkubwa. Formula One dhidi ya Formular Three.
‘Kwa sasa, wapo vizuri zaidi na unaweza kuona hilo kirahisi zaidi, hivyo
ni vigumu sana kuwajaji wachezaji wangu. Hata kwenye masuala kama haya,
unaweza kupata wachezaji watatu, wanne au watano. Vinginevyo ni vigumu
sana japo unaweza kuona ubora uliopo.”
Saturday, 23 July 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment