Wakati serikali ikiendelea kuhakikisha vyeti kubaini watumishi wasiokuwa
na sifa, watu wengi wamejitokeza kutangaza kupotelewa na vyeti
magazetini
Katika kipindi ambacho taasisi mbalimbali zinaendelea na zoezi hilo
imebainika kuwa siku za nyuma kulikuwa na matangazo ya aina tofauti
lakini kwa juzi kumetokea mtiririko wa watu kutangaza kupotelewa na
vyeti hali isiyo ya kawaida kwa taifa.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Ufundi , Profesa Joyce
Ndalichako alisema juzi kuwa serikali itafanya uhakiki wa vyeti katika
vyuo na sehemu za kazi.
Naye Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)Godius
Kahyarara juzi alitoa waraka akisema wafanyakazi watakaoshindwa
kuwasilisha vyeti vyao halisi hawatalipwa mishahara.
Saturday, 23 July 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment