Watu tisa wameuawa na wengine 10
kujeruhiwa baada ya watu wenye bunduki waliowafyatulia risasi watu
katika jumba moja la kibiashara mjini Munich, Ujerumani.
Polisi wanasema washukiwa bado hawajakamatwa na wamewatahadharisha watu na kuwashauri kutotoka nje.Wanachunguza iwapo mmoja wa waliofariki ni mtuhumiwa.

Operesheni kubwa ya kiusalama inaendelea katika jumba la kibiashara la Olympia, ambalo linapatikana mtaa wa Moosach, kaskazini magharibi mwa Munich.
Maafisa wa polisi jimbo la Bavaria wamekuwa katika hali ya tahadhari tangu Jumatatu kijana mhamiaji alipowadunga visu na kuwajeruhi watu kadha katika treni, shambulio ambalo kundi la Islamic State lilidai kuhusika.
Polisi wamesema shambulio hilo ni la kigaidi.
0 comments:
Post a Comment